Slide Title 1

Aenean quis facilisis massa. Cras justo odio, scelerisque nec dignissim quis, cursus a odio. Duis ut dui vel purus aliquet tristique.

Slide Title 2

Morbi quis tellus eu turpis lacinia pharetra non eget lectus. Vestibulum ante ipsum primis in faucibus orci luctus et ultrices posuere cubilia Curae; Donec.

Slide Title 3

In ornare lacus sit amet est aliquet ac tincidunt tellus semper. Pellentesque habitant morbi tristique senectus et netus et malesuada fames ac turpis egestas.

Saturday, March 8, 2014

wali wa asumini


Mchele kilo 1
Kuku mkubwa 1
Vitunguu maji kilo 2
Mayai 8
Samli kilo 1
Thomu gram 200
Tangawizi mbichi gram 50
Mdalasini gram 50
Hiliki gram 50
Bizari nzima kiasi
Siki kiasi
Mtindi painti 1
Tungule kilo 1
Zabibu nyeusi kiasi
1    Mkate kuku umwoshe umchemshe kwa maji na chumvi mpaka awive, kisha muepue.
2    Menya vitunguu uvioshe uvikate na uvigawe sehemu mbili. Sehemu moja uiweke, sehemu        ya pili vikaange mpaka       viwe vyekundu kama vya biriani. Kisha vichuje uitoe         samli yote, vitie katika sinia uvitandaze ili vipoe kwa kupata           upepo.
3   Chukua mdalasini, hiliki na bizari utwange pamoja, kisha uchunge unga laini. Saga         thomu na tangawizi mbichi. Saga      tungule.
4   Teleka sufuria tia samli ile ile iliyokaangiwa vitunguu halafu utie vile vitunguu         vilivyobakia uvikaange. Vikianza kuiva          tia viungo ulivyovitwanga na             kuvisaga. (Bakisha vitunguu na viungo kidogo). Tia vipande vya kuku, mtindi  siki na        supu ya kuku iliyobakia katika sufuria. Acha ichemke nyama pamoja na vitu vyote       mpaka libaki rojorojo.
5   Teleka maji, yakichemka tia chele. Ukiiva utoe uchuje yatoke maji yote.
6   Teleka tena sufuria utie samli kidogo utie na vile vitunguu ulivyovibakisha               uvikaange. Tia mdalasini nzima, kaanga          pamoja, tia na ule wali ukoroge           koroge ili uchanganyike na viungo. Kisha ufunike upalie moto.
7   Chemsha mayai yote uyamenye.
8   Wali ukishakauka utaupakua, lakini lazima itabidi utumie kombe au sahani kubwa           itakayoweza kuingia wali pamoja na vitu vyote. Kuupakua kwake kwanza utatia nusu ya       wali katika hiyo sahani, baadae utatia masalo na nyama yote, na mayai, kisha             utayafunika masalo kwa wali uliobakia. Mwisho utachukua vile vitunguu ulivyovikaanga     na ukavitandaza ili vipo, utavimwaga juu ya wali.Kwani ni kwa sababu ya hivi vitunguu     ndio maana ukaitwa wali wa asumini. Ukipenda utapamba chembe za zabibu juu yake.         ZABIBU HIZO Ziroweke kwanza ili zivimbe.

pishi la sambusa


Mahitaji
Unga wa ngano    ½
Viazi Ulaya    ¼kg 
Maji ya uvuguvugu kiasi
Kitunguu saumu kilichosagwa kijiko 1 kikubwa 
Tangawizi     kiasi
Pilipili mbuzi     1 (kama unatumia)
Vitunguu maji        3
Viungo            kiasi
Chumvi        kiasi
Njegere mbichi kikombe 1
Chumvi kiasi
Unga wa ngano vijiko 3 vya chakula.

Namna ya kutengeza

Chukua unga wa ngano ½ kg na kanda hadi ulainike kama unavyofanya kwa unga wa maandazi.
Baada ya hapo chukua mbogamboga zote katakata vipande vidogovidogo na kisha weka chumvi na baadaye viungo vya unga,kisha weka jikoni. 
Baaada ya dakika tano ipua na weka chini.

Gawa unga ulioukanda katika sehemu kumi. Tandaza kidogo,  kisha paka mafuta juu yake. Sukuma kama chapati,  kisha weka kwenye chuma cha kukaangia chapati bila ya kuweka mafuta.
Baada ya kubabua weka kwenye kibao cha chapati na kisha kata sehemu nne.
  
Chukua unga wa ngano vijiko 3 vya mezani na kisha tengeneza uji mzito kwa ajili ya kugandisha sambusa zako. 
Tengeneza umbo la koni kutoka kila kipande cha chapati ulichokata. Jaza mchanganyiko wa mbogamboga ndani yake. Funga sehemu ya juu, kwa kugandisha na uji uliotengeneza.

Fanya hivyo hadi chapatti zote ziishe. Chukua mafuta na weka jikoni, yakipata moto weka sambusa zako. Kaanga hadi ziwe rangi ya hudhurungi.


Ipua na chuja mafuta katika chujio la bati. Baada ya hapo sambusa zako zitakuwa tayari kuliwa.

vitumbua


Mahitaji:
  • Unga wa mchele ½ kg
  • Sukari vijiko 4 vya mezani
  • Tui bubu la nazi
  • Mafuta ya kupikia
  • Unga wa hiliki ½ kijiko cha chai
  • Hamira kijiko 1 cha chai
  • Chuma cha vitumbua
Maandalizi:
  • Chukua unga wa mchele na weka kwenye bakuli au sufuria ya kilo moja
  • Weka hamira kisha weka sukari kisha miminia tui katika mchanganyiko wako
  • Weka hiliki koroga hadi view uji mzito
  • Acha uji huo kwa muda wa saa moja hadi uumuke, mara nyingi kuumuka kunategemea na hali ya hewa,
  • Baada ya hapo weka mafuta kijiko kimoja cha chakula kila kishimo acha yapate moto

biringanyi ya mbogamboga


Mahitaji:
  • ½ kg mchele wa basmati
  • Kitunguu maji kikubwa 1
  • Nyanya 1 kubwa
  • Karoti 1 kubwa
  • Njegere robo kikombe
  • Kiazi ulaya 1 kikubwa
  • Tangawizi za kusaga kijiko 1
  • Kitunguu swaumu cha kusaga kijiko 1
  • Karafuu kijiko 1
  • Majani ya kotimili fungu 1
  • Maziwa ya mtingi ¼ kikombe
  • Chumvi na pilipili kiasi
  • Unga wa dhani kijiko 1 cha mezani
  • Juisi ya limao kijiko 1 cha mezani
  • Mafua ¼ lita
Maandalizi:
  • Chemsha mchele na kisha weka pembeni
  • Osha mbogamboga zote isipokuwa vitunguu na nyanya
  • Changanya mtindi na tangawizi pamoja na kitunguu swaumu viache vikae kwa muda wa saa moja
  • Chukua sufuria weka mafuta na kisha kaanga vitunguu maji, weka nyanya, chumvi, kotimili na limao halafu weka karafuu na kanga hadi vichanganyike vizuri
  • Miminia mchanganyiko wa mtindi na baadaye weka pilipili na baadaye weka unga wa dhania
  • Chukua mchele uliochemshwa changanya na mchanganyiko huo
  • Palia moto juu ya chakula chako na acha kwa muda wa dakika 30
  • Baada ya hapo chakula chako cha biriani kitakuwa tayari kwa kuliwa

roast ya biringanyi na mayai


Mahitaji:
Biringanya 2 kubwa
Nyanya 4 kubwa
Kitunguu maji kilichosagwa kijiko 1 cha mezani
Mayai 2
Mafuta ya mzeituni vijiko vitatu vya mezani
Chumvi kiasi
Pilipili 1 (kama unatumia)
Hoho 1
Karoti 1
Kitunguu swaumu kilichosagwa 1
Kotimili fungu 1

Maadalizi:
Chukua biringanya ioshe vizuri na kasha katakata vipande vidogo vidogo.
Osha na menya nyanya hapafu katakata. Fanya hivyo kw akaroti na hoho pia.
Weka mafuta kwenye sufuria na weka jikoni kwenye moto kiasi
Yakishachemka maji na kasha weka kitunguu maji na kasha swaumu huku ukikaanga taratibu.
Weka hoho na karoti huku ukiendelea kukaanga. Baada ya hapo weka nyanya na baadae chumvi. Funika hadi ziive kabisa na kasha weka majani ya kotimili.
Weka biringanya. Acha vichemke hadi viive. Koroga ili kuruhusu mchanganyiko wako uchanganyike vizuri.
Kwa kuwa biringanya ina majimaji huhitaji kuweka maji ya ziada, weka pilipili.
Acha kwa muda wa dakika tatu hadi dakika tano. Pasua mayai na kisha miminia huku ukikoroga taratibu. Fanya hivyo hadi yaive kabisa na kuwa mchuzi mzito. Roast yako ya biringanya iko tayari kwa kuliwa
Unaweza kula aina hii ya mboga na mikate, maandazi na hata ugali

salad ya matunda


Mahitaji
Embe iliyoiva kiasi
Nanasi
Tango
Tikiti maji
Zabibu
Papai

Matayarisho

1. Ondoa maganda kwenye embe, nanasi, tango, papai na tikiti maji kisha kata kata vipande vidogo vidogo vya mraba

2. Changanya vipande vya matunda kwenye bakuli safikisha weka na zabibu zilizotolewa kwenye kikonyo chake.

3. Weka kwenye friji yapate ubaridi kidogo

4. Saladi yako tayari kwa kuliwa

Waweza kula saladi hii kama mlo wa kati au kama mlo kamili wa usiku.


Mapishi – Mayai Mchanganyiko, Tosti na Soseji


Mahitaji
Mayai 3
Soseji 2
Mkate slesi 2
Mafuta ya kupikia vijiko 2
Chumvi

Matayarisho
Piga piga mayai vizuri kwenye bakuli na weka chumvi kidogo kisha weka kikaango kwenye moto na mafuta kidogo.

Kikisha pata moto miminia mchanganyiko wa mayai na uanze kukorogo pale tu unapomiminia, endelea kukoroga hadi uone yanakuwa magumu na kuanza kuiva. Pika kwa kiwango unachopendelea na kusha epua na weka kwenye sahani.

Weka mafuta kijiko kimoja kwenye kikaango na kisha weka soseji zako na uzipike kiasi pande zote kisha epua na weka pembeni.

Weka slesi za mikate kwenye toster na zikiwa tayari unaweza weka siagi ili kuongeza ladha na mvuto.
Andaa mlo wako pamoja na juice, maziwa au chai.